Miss Arusha City Center kujulikana Mei 5

Washiriki wa kitongoji Kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja, tayari kuchuana vikali Mei 5, 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii, Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha. Katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000 na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000.

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi, Modern Driving School, ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.

Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji Kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2012, yanatarajiwa kufanyika Mei 5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii, Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.

Akizungumza leo jijini Arusha, Mratibu wa shindano hilo Bi. Upendo Simwita kutoka kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa wametimia 20.

Bi Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki, anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya ushindani, kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.

“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20, ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center,” alisema Upendo. Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh. 25,000 na kwa viti vya kawaida sh. 15,000. Fanya booking yako ya tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.

Kwa upande wa Burudani, Upendo amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli, Muziki wa Asili, Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.

Upendo amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S ORIGINAL, NAURA SPRINGS HOTEL, CLAUDS FM /CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB – ARUSHA, BG HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL, MAKO ADVENTURE, SEBE & BEKI FOR LIFE, MWANDAGO INVESTMENT, S. G. RESORT, MEJA LINK LTD, GEO SECURITY, GOLDEN ROSE HOTEL, RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES, ARUSHA TRAVEL LODGE, LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA, WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY PAURLOR NA HADIJA HAS

 

 

 

Advertisements
Hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Mizengo pinda , kwa mujibu wa katiba Ibara ya 53A, na kanuni ya bunge, Kifungu cha 133 kuwasilishwa kwa spika leo.

hatahivyo tayari wabunge 73 wazalendo washasaini katika daftari hilo, ambapo inaelezwa kuwa ni mwendelezo wa operesheni ya uwajibikaji, Naibu kiongozi kambi ya upinzani Bungeni zitto kabwe akisisitiza.

  • Asisitiza ushirika hujenga dunia iliyo bora.

 Na Belinda Masangula na Shani Ramadhani  TLC

RAISI  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh. Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi katika jengo la ushirika linalotarajiwa kujengwa karibu na jengo la zamani la ushirika ambalo lilijengwa mwaka 1964.

Zoezi hilo limefanyika wakati wa uzinduzi rasmi wa mwaka wa kimataifa wa vyama vya ushirika uliyofanyika mkoani Dar es Salaam mapema mwezi huu.

 

Akizungumza na wanachama wa vyama vya ushirika waliokusanyika mahali hapo raisi Kikwete alisema endapo ushirika utastawi na kuimarika hali ya maisha itakuwa bora kutokana na ukweli kwamba ushirika umejengeka juu ya dhana isemayo umoja ni nguvu.

“Ushirika hujenga dunia iliyo bora hivyo kupitia ushirika watu wanakusanyika pamoja ili kufanya shughuli za kiuchumi zitakazowaongezea mapato ili kuinua hali zao za maisha,” alisisitiza.

Akizungumza  Mh. Kikwete alibainisha uwepo wa vyama vya ushirika nje na ndani ya bara la Afrika zikiwemo nchi tajiri na maskini na katika nchi zilizoendelea ulianza mwaka 1761, miaka 251 iliyopita ambapo hapa nchini ushirika ulianza mwaka 1925 na chama cha wakulima cha Kilimanjaro Network Zantez Association (KNZA) na baadae mwaka 1933 kubadilishwa kuwa Kilimanjaro Network Cooperation Union ( KNCU).

“Chimbuko la ushirika duniani kote ni dhamira ya wanyonge kukusanya nguvu zao ili upambana na dhuluma ambapo kichocheo kikubwa cha kuanzisha mwaka wa ushirika kilikuwa ni dhuluma waliyokuwa wanafanyiwa wakulima na wanfanyabiashara binafsi,” alieleza.

Aidha raisi Kikwete alieleza kwamba ushirika ulikuwa ni chombo cha kuwakomboa kutokana na unyonyaji waliyopkuwa wakikumbana nao ambapo kazi kubwa ya vyama vya ushirika ilikuwa ni kununua mazao ya wakulima,kukuza na kuunda chombo cha mkulima jambo ambao linaaminika kuwa lilisaidia wakulima kupata elimu,pembejeo,rasiliamali zao kwa gharama nafuu,kupata huduma zilizokuwa zikikosekana na kusisitiza kwamba kutokana na hayo vyama vya ushirika vilikuwa mkombozi na vilipendwa na kutumainiwa na wakulima kwani viliwasaidia pia kupata dawa za kinga za mazao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa vyama vya ushirika Bw.Gorge kahama alieleza kwamba maudhui ya kuwepo na vyama vya ushirika duniani ni kukuza uelewa wa umma kuhusu kukuza vyama vya ushirika na mchango wake katika Nyanja za kiuchumi na kijamii kwa mtu mmoja mmoja, jamii,kitaifa na kimataifa na kuhamasisha wanacnhi kutumia ushirika kama njia ya kujikwanua kiuchumi na kijamii aidha kwakuvijengea uwezo vyama hivyo ili kuongeza ufanisi wakazi zake na wadau kuibua mapendekezo ya kisheria kw aajili ya kujenga mazimgira bora ya maendeleo yake

 

Aidha mwenyekiti huyo alisema kuwa shirika linatumia maadhimisho hayo kuimarisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika vilivyopo na kustawisha vilivyoimarika na  kuwahamasisha watu, jamii, idara za serikali katika kutambua utawala wa vyama vya kitaifa katika kulisaidia taifa kufikia malengo ya kitaifa kama vile mkukuta na program ya kilimo kwanza.

Pia mwenyekiti huyo alisema kuwa shirika linaomba serikali kuboresha miundombinu itakayowezesha kusafirisha mazao kwa sabau wanaushirika wengi ni wakulima na wanategemea kilimo hivyo wajengewe barabara ili kusafirisha mazao yao pia shirikisho limeomba wakulima wapewe hakimiliki ya mashamba ili waendeleze kilimo.

Aidha mwenyekiti huyo alisema kuwa bei hiyo ya mazo ya korosho  imekuwa ikipanda na kushuka na hivyo shirikisho linaomba serikali kutoa stakabdhi ya mazao hayo ili kuwasaidia wakulima kunufaika na mazao yao.

Pia mwenyekiti huyo alisema vyama vya ushirika na mikopo vimekuwa vikiwasaidia wanannchi kujikawamua katika maisha na hivyo mwenyekiti huyo kutoa wito kwa serikali kutovitoza kodi kubwa vyama vya ushirika na mikopo  ili faida ndogo inayopatikana katika vyama iweze kuendeleza nakukuza vyama hivyo vya ushirika.

Vyama vya ushirika vilikuwa na kauli iliyosikilizwa ambapo TANU iliamua kuwa karibu sana na vyama vya ushirika katika kudai uhuru wa Tanzania ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi. Vyama vya ushirika viliendelea vizuri sana miaka kumi baada ya uhuru.

MWISHO.

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Maliasili na Utalii inawakambusha wananchi wote kuwa tarehe Mosi Aprili kila mwaka ni SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI. Mwaka huu maadhimisho ya kitaifa yatafanyika mkoani Singida. Kama ilivyo kawaida tarehe Mosi Aprili ni siku ya uhamasishaji, na kila mwananchi anatakiwa kupanda miti michache kama hakutakuwa na mvua za kutosha. Miti mingine ipandwe wakati muafaka kadri majira ya mvua yatakavyoruhusu. Chimbuko la Siku ya Taifa ya Kupanda Miti ilikuwa ishara ya kuikaribisha Milenia mpya kwa kupanda miti ambapo Serikali iliwahamasisha wananchi kupanda miti milioni mia moja mwanzoni mwa mwaka 2000. Mwaka huo huo wa 2000 Waziri Mkuu ilitoa Waraka wa Serikali Namba 1 wa mwaka 2000 ambao ulielekeza kuwa Januari mosi kila mwaka ni Siku ya Taifa ya Kupanda Miti. Hata hivyo, kwa kutambua kuwa siyo kila mkoa unapata mvua mwezi Januari Waziri Mkuu alitoa waraka mwingine Namba 1 wa mwaka 2009 ambao uliibadili Siku ya Taifa ya Kupanda Miti kutoka tarehe mosi Januari kuwa tarehe mosi Aprili kila mwaka. Wizara inasisitiza kuwa mwaka huu shughuli za kupanda miti zitaambatana na kutenga maeneo na kuyatunza ili miti ya asili iweze kuota yenyewe. Njia hii imefanikisha maendeleo ya misitu mkoani Shinyanga ambapo wananchi wanastawisha misitu kwa kutumia uoto wa asili, njia ijulikanayo kama ‘ngitili’.

George Matiko

MSEMAJI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

26 Machi 2012

BARAZA la Habari Tanzania (MCT) umekamilisha mitaala kwa vyuo vya uandishi wa habari nchini. Mitaala hiyo imegawanyika katika ngazi kuu tatu, TA level 4 ngazi ya Basic Certificate, TA lever 5 kwa Advance Certificate na TA level  6 kwa ngazi ya Diploma.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa baraza la habari Tanzania Bw.Kajubi Mkajanga katika ziara yake ya kutembelea vyuo vya habari vilivyopo hapa nchini ,alisema  kuwa wamechukua  miaka miwili kuandaa mitaala na kuwashilikisha  wataalam wakiwemo train ya vyuo vya taasisi ya uwekezaji wa mitaala, na kuwahusisha na nacte ambao ni baraza la Taifa elimu ya ufundi na usajili wa hivi vyuo.

Hivyo basi tukaona ni bora kabla ya kugawa mitaala vyuoni ni kutembelea kila vyuo na kuona ni jinsi gani ya kuweza kutoa mitaala kwa ufasasaha zaidi na vigezo ambavyo wanazingatia katika mitaala hiyo.Pia vigezo ambavyo vinazinagtiwa zaidi ni kwa kuangalia walimu wana vigezo vinavyotakiwa kwa kuweza kutumia mitaala hii.

Tumeanzia  Zanzibar,Morogoro,Iringa na sasa tupo Dar es salaam ambapo tutatembelea TSJ, DSJ na Royal na mwisho tunamalizia na Arusha.Kwa kufanya hivi tutagundua vyuo vipi vina mapungufu na havipaswi kupewa mitaala hii,

Pia alizungumzia pia kwa upande wa wanafunzi wanao chukuliwa hapo vtuoni je wanavigezo gani,kwa kufanya hivi kutasaidia mitaala tuiogawayo atutoi kimakosa  bali tunaangalia vigezo zaidi kwa kumjenga mwalimu na mwanafunzi kuwa ktika kiwango kizuri katika fani hii ya uandishi kwa ujumla.

Aliendelea kufafanua kuwa hawatatoa mitaala bure bali kila mtaala utagharim shilingi milioni moja na nusu hivyo basi kwa mitaala mitatu kwa shilingi million nne na nusu.kwa kufanya hivi tunaomba kilia vyuo vitambue kuwa hakuna ruzuku vifanye biashara na kusonga mbele zaidi.

“amesisitiza kuwa vyuo vinatakiwa vifanye biashara ili utamaduni wa ruzuku uishe. Mfano mzuri ni mradi uliopo TSJ ni njia mojawapo ya kusonga mbele”

Pia aliwashauri wazazi kuwa wawe tayari kuwapeleka watoto wao vyuoni ili kupata elimu bora ya uandishi kwa ufasaha, kwani ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mtoto anapata maadili mema  zaidi.

“Tunapata changamoto mbalimbali ikiwemo ya maadili kwa waandishi wa habari, wahariri kuelewa kitu kinachozungumziwa na mvutano kati ya serikali na waandishi hivyo kila changamoto ni kama fursa na tunaifanyia kazi”alisema Mwakajanga

Naye Mkurugenzi wa chuo cha Uandishi wa habari wa TIME Bw. Kiondo Mshana amesema kuwa mradi wa TLC una lengo la kuibua vipaji kwa waandishi wa habari na kwa vitendo zaidi hususani katika vipengele mbalimbali kama Uandishi wa magazeti (Super brain) Upigaji picha(Tree media), Utangazaji Radio na Runinga (Maa Media), na elimu ya uandishi kupitia  Mitandao (Jamii forum)

Na mwisho wa yote naye Afisa masoko wa mradi huo Mh. Dastan Kamanzi, amesema kuwa kituo kinatoa mafunzo bora kwa vitendo  pia kinahusisha wanafunzi wa nazi ya cheti na stashahada ambapo mradi huo ulianzishwa mwaka jana na bado una malengo mengi kwa wanfunzi .Hivyo basi alitoa wito kwa wanafunzi wote na kuwahasa sana kuzingatia mafunzo kwa ufasaha zaidi.

MWISHO