Archive for March, 2012

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Maliasili na Utalii inawakambusha wananchi wote kuwa tarehe Mosi Aprili kila mwaka ni SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI. Mwaka huu maadhimisho ya kitaifa yatafanyika mkoani Singida. Kama ilivyo kawaida tarehe Mosi Aprili ni siku ya uhamasishaji, na kila mwananchi anatakiwa kupanda miti michache kama hakutakuwa na mvua za kutosha. Miti mingine ipandwe wakati muafaka kadri majira ya mvua yatakavyoruhusu. Chimbuko la Siku ya Taifa ya Kupanda Miti ilikuwa ishara ya kuikaribisha Milenia mpya kwa kupanda miti ambapo Serikali iliwahamasisha wananchi kupanda miti milioni mia moja mwanzoni mwa mwaka 2000. Mwaka huo huo wa 2000 Waziri Mkuu ilitoa Waraka wa Serikali Namba 1 wa mwaka 2000 ambao ulielekeza kuwa Januari mosi kila mwaka ni Siku ya Taifa ya Kupanda Miti. Hata hivyo, kwa kutambua kuwa siyo kila mkoa unapata mvua mwezi Januari Waziri Mkuu alitoa waraka mwingine Namba 1 wa mwaka 2009 ambao uliibadili Siku ya Taifa ya Kupanda Miti kutoka tarehe mosi Januari kuwa tarehe mosi Aprili kila mwaka. Wizara inasisitiza kuwa mwaka huu shughuli za kupanda miti zitaambatana na kutenga maeneo na kuyatunza ili miti ya asili iweze kuota yenyewe. Njia hii imefanikisha maendeleo ya misitu mkoani Shinyanga ambapo wananchi wanastawisha misitu kwa kutumia uoto wa asili, njia ijulikanayo kama ‘ngitili’.

George Matiko

MSEMAJI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

26 Machi 2012

Advertisements

BARAZA la Habari Tanzania (MCT) umekamilisha mitaala kwa vyuo vya uandishi wa habari nchini. Mitaala hiyo imegawanyika katika ngazi kuu tatu, TA level 4 ngazi ya Basic Certificate, TA lever 5 kwa Advance Certificate na TA level  6 kwa ngazi ya Diploma.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa baraza la habari Tanzania Bw.Kajubi Mkajanga katika ziara yake ya kutembelea vyuo vya habari vilivyopo hapa nchini ,alisema  kuwa wamechukua  miaka miwili kuandaa mitaala na kuwashilikisha  wataalam wakiwemo train ya vyuo vya taasisi ya uwekezaji wa mitaala, na kuwahusisha na nacte ambao ni baraza la Taifa elimu ya ufundi na usajili wa hivi vyuo.

Hivyo basi tukaona ni bora kabla ya kugawa mitaala vyuoni ni kutembelea kila vyuo na kuona ni jinsi gani ya kuweza kutoa mitaala kwa ufasasaha zaidi na vigezo ambavyo wanazingatia katika mitaala hiyo.Pia vigezo ambavyo vinazinagtiwa zaidi ni kwa kuangalia walimu wana vigezo vinavyotakiwa kwa kuweza kutumia mitaala hii.

Tumeanzia  Zanzibar,Morogoro,Iringa na sasa tupo Dar es salaam ambapo tutatembelea TSJ, DSJ na Royal na mwisho tunamalizia na Arusha.Kwa kufanya hivi tutagundua vyuo vipi vina mapungufu na havipaswi kupewa mitaala hii,

Pia alizungumzia pia kwa upande wa wanafunzi wanao chukuliwa hapo vtuoni je wanavigezo gani,kwa kufanya hivi kutasaidia mitaala tuiogawayo atutoi kimakosa  bali tunaangalia vigezo zaidi kwa kumjenga mwalimu na mwanafunzi kuwa ktika kiwango kizuri katika fani hii ya uandishi kwa ujumla.

Aliendelea kufafanua kuwa hawatatoa mitaala bure bali kila mtaala utagharim shilingi milioni moja na nusu hivyo basi kwa mitaala mitatu kwa shilingi million nne na nusu.kwa kufanya hivi tunaomba kilia vyuo vitambue kuwa hakuna ruzuku vifanye biashara na kusonga mbele zaidi.

“amesisitiza kuwa vyuo vinatakiwa vifanye biashara ili utamaduni wa ruzuku uishe. Mfano mzuri ni mradi uliopo TSJ ni njia mojawapo ya kusonga mbele”

Pia aliwashauri wazazi kuwa wawe tayari kuwapeleka watoto wao vyuoni ili kupata elimu bora ya uandishi kwa ufasaha, kwani ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mtoto anapata maadili mema  zaidi.

“Tunapata changamoto mbalimbali ikiwemo ya maadili kwa waandishi wa habari, wahariri kuelewa kitu kinachozungumziwa na mvutano kati ya serikali na waandishi hivyo kila changamoto ni kama fursa na tunaifanyia kazi”alisema Mwakajanga

Naye Mkurugenzi wa chuo cha Uandishi wa habari wa TIME Bw. Kiondo Mshana amesema kuwa mradi wa TLC una lengo la kuibua vipaji kwa waandishi wa habari na kwa vitendo zaidi hususani katika vipengele mbalimbali kama Uandishi wa magazeti (Super brain) Upigaji picha(Tree media), Utangazaji Radio na Runinga (Maa Media), na elimu ya uandishi kupitia  Mitandao (Jamii forum)

Na mwisho wa yote naye Afisa masoko wa mradi huo Mh. Dastan Kamanzi, amesema kuwa kituo kinatoa mafunzo bora kwa vitendo  pia kinahusisha wanafunzi wa nazi ya cheti na stashahada ambapo mradi huo ulianzishwa mwaka jana na bado una malengo mengi kwa wanfunzi .Hivyo basi alitoa wito kwa wanafunzi wote na kuwahasa sana kuzingatia mafunzo kwa ufasaha zaidi.

MWISHO