siku ya taifa ya kupanda miti kuadhimishwa Singida tarehe 1April 2012

Posted: March 27, 2012 in Uncategorized

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Maliasili na Utalii inawakambusha wananchi wote kuwa tarehe Mosi Aprili kila mwaka ni SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI. Mwaka huu maadhimisho ya kitaifa yatafanyika mkoani Singida. Kama ilivyo kawaida tarehe Mosi Aprili ni siku ya uhamasishaji, na kila mwananchi anatakiwa kupanda miti michache kama hakutakuwa na mvua za kutosha. Miti mingine ipandwe wakati muafaka kadri majira ya mvua yatakavyoruhusu. Chimbuko la Siku ya Taifa ya Kupanda Miti ilikuwa ishara ya kuikaribisha Milenia mpya kwa kupanda miti ambapo Serikali iliwahamasisha wananchi kupanda miti milioni mia moja mwanzoni mwa mwaka 2000. Mwaka huo huo wa 2000 Waziri Mkuu ilitoa Waraka wa Serikali Namba 1 wa mwaka 2000 ambao ulielekeza kuwa Januari mosi kila mwaka ni Siku ya Taifa ya Kupanda Miti. Hata hivyo, kwa kutambua kuwa siyo kila mkoa unapata mvua mwezi Januari Waziri Mkuu alitoa waraka mwingine Namba 1 wa mwaka 2009 ambao uliibadili Siku ya Taifa ya Kupanda Miti kutoka tarehe mosi Januari kuwa tarehe mosi Aprili kila mwaka. Wizara inasisitiza kuwa mwaka huu shughuli za kupanda miti zitaambatana na kutenga maeneo na kuyatunza ili miti ya asili iweze kuota yenyewe. Njia hii imefanikisha maendeleo ya misitu mkoani Shinyanga ambapo wananchi wanastawisha misitu kwa kutumia uoto wa asili, njia ijulikanayo kama ‘ngitili’.

George Matiko

MSEMAJI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

26 Machi 2012

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s