Posts Tagged ‘jakaya kikwete’

  • Asisitiza ushirika hujenga dunia iliyo bora.

 Na Belinda Masangula na Shani Ramadhani  TLC

RAISI  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh. Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi katika jengo la ushirika linalotarajiwa kujengwa karibu na jengo la zamani la ushirika ambalo lilijengwa mwaka 1964.

Zoezi hilo limefanyika wakati wa uzinduzi rasmi wa mwaka wa kimataifa wa vyama vya ushirika uliyofanyika mkoani Dar es Salaam mapema mwezi huu.

 

Akizungumza na wanachama wa vyama vya ushirika waliokusanyika mahali hapo raisi Kikwete alisema endapo ushirika utastawi na kuimarika hali ya maisha itakuwa bora kutokana na ukweli kwamba ushirika umejengeka juu ya dhana isemayo umoja ni nguvu.

“Ushirika hujenga dunia iliyo bora hivyo kupitia ushirika watu wanakusanyika pamoja ili kufanya shughuli za kiuchumi zitakazowaongezea mapato ili kuinua hali zao za maisha,” alisisitiza.

Akizungumza  Mh. Kikwete alibainisha uwepo wa vyama vya ushirika nje na ndani ya bara la Afrika zikiwemo nchi tajiri na maskini na katika nchi zilizoendelea ulianza mwaka 1761, miaka 251 iliyopita ambapo hapa nchini ushirika ulianza mwaka 1925 na chama cha wakulima cha Kilimanjaro Network Zantez Association (KNZA) na baadae mwaka 1933 kubadilishwa kuwa Kilimanjaro Network Cooperation Union ( KNCU).

“Chimbuko la ushirika duniani kote ni dhamira ya wanyonge kukusanya nguvu zao ili upambana na dhuluma ambapo kichocheo kikubwa cha kuanzisha mwaka wa ushirika kilikuwa ni dhuluma waliyokuwa wanafanyiwa wakulima na wanfanyabiashara binafsi,” alieleza.

Aidha raisi Kikwete alieleza kwamba ushirika ulikuwa ni chombo cha kuwakomboa kutokana na unyonyaji waliyopkuwa wakikumbana nao ambapo kazi kubwa ya vyama vya ushirika ilikuwa ni kununua mazao ya wakulima,kukuza na kuunda chombo cha mkulima jambo ambao linaaminika kuwa lilisaidia wakulima kupata elimu,pembejeo,rasiliamali zao kwa gharama nafuu,kupata huduma zilizokuwa zikikosekana na kusisitiza kwamba kutokana na hayo vyama vya ushirika vilikuwa mkombozi na vilipendwa na kutumainiwa na wakulima kwani viliwasaidia pia kupata dawa za kinga za mazao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa vyama vya ushirika Bw.Gorge kahama alieleza kwamba maudhui ya kuwepo na vyama vya ushirika duniani ni kukuza uelewa wa umma kuhusu kukuza vyama vya ushirika na mchango wake katika Nyanja za kiuchumi na kijamii kwa mtu mmoja mmoja, jamii,kitaifa na kimataifa na kuhamasisha wanacnhi kutumia ushirika kama njia ya kujikwanua kiuchumi na kijamii aidha kwakuvijengea uwezo vyama hivyo ili kuongeza ufanisi wakazi zake na wadau kuibua mapendekezo ya kisheria kw aajili ya kujenga mazimgira bora ya maendeleo yake

 

Aidha mwenyekiti huyo alisema kuwa shirika linatumia maadhimisho hayo kuimarisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika vilivyopo na kustawisha vilivyoimarika na  kuwahamasisha watu, jamii, idara za serikali katika kutambua utawala wa vyama vya kitaifa katika kulisaidia taifa kufikia malengo ya kitaifa kama vile mkukuta na program ya kilimo kwanza.

Pia mwenyekiti huyo alisema kuwa shirika linaomba serikali kuboresha miundombinu itakayowezesha kusafirisha mazao kwa sabau wanaushirika wengi ni wakulima na wanategemea kilimo hivyo wajengewe barabara ili kusafirisha mazao yao pia shirikisho limeomba wakulima wapewe hakimiliki ya mashamba ili waendeleze kilimo.

Aidha mwenyekiti huyo alisema kuwa bei hiyo ya mazo ya korosho  imekuwa ikipanda na kushuka na hivyo shirikisho linaomba serikali kutoa stakabdhi ya mazao hayo ili kuwasaidia wakulima kunufaika na mazao yao.

Pia mwenyekiti huyo alisema vyama vya ushirika na mikopo vimekuwa vikiwasaidia wanannchi kujikawamua katika maisha na hivyo mwenyekiti huyo kutoa wito kwa serikali kutovitoza kodi kubwa vyama vya ushirika na mikopo  ili faida ndogo inayopatikana katika vyama iweze kuendeleza nakukuza vyama hivyo vya ushirika.

Vyama vya ushirika vilikuwa na kauli iliyosikilizwa ambapo TANU iliamua kuwa karibu sana na vyama vya ushirika katika kudai uhuru wa Tanzania ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi. Vyama vya ushirika viliendelea vizuri sana miaka kumi baada ya uhuru.

MWISHO.

Advertisements